Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) 2018, yameanza kutimua vumbi leo hii 4 Juni, 2018, katika vituo viwili vya chuo cha ualimu Butimba na Nsumba Sekondari jijini Mwanza.
Timu ya Mkoa wa Rukwa ikiliandama goli la Timu ya Mwanza katika kipindi cha pili baada ya kwenda mapunziko wakiwa nyuma magoli 23 kwa 6 |
Timu ya Mkoa wa Mwanza ikifunga moja kati ya magoli yake iliyopata katika mchezo wake dhidi ya Rukwa, pembeni ni mashabiki kindakindaki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo. |
Katika michezo mingine ya mchezo huo iliyopigwa katika viwanja tofauti vya vituo hivyo timu ya mkoa wa Tabora wanawake iliweza kuichapa Timu ya Arusha kwa magoli 27 kwa 18, huku timu ya mkoa wa Katavi ikiichapa timu ya Pwani kwa magoli 24 kwa 17.
0 comments:
Post a Comment