Marco Asensio |
Chelsea imewasilisha ombi la dau la £35m kumnunua beki wa Juventus Daniele Rugani, 23. Klabu hiyo inatumai kwamba raia huyo wa Italia atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na mkufunzi Maurizio Sarri. (Evening Standard)
Marouane Fellaini |
Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini atatoa tangazo kuhusu hatma yake mnamo tarehe mosi mwezi Julai. Raia huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 30 hajakubaliana na masharti ya klabu hiyo kuhusu mkataba mpya. (Manchester Evening News)
Jack Grealish, 22, yuko tayari kuondoka Aston Villa msimu huu ili kurudi katika ligi kuu ya Uingereza, huku Tottenham ikiongoza katika kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Uingereza (Mirror)
Sokratis Papastathopoulos |
Arsenal inakaribia kumsaini beki wa Borussia Dortmund Sokratis Papastathopoulos, 30, huku ikiendelea na mazungumzo ya kutaka kumsajili beki wa Freiburg na Uturuki Caglar Soyuncu, 22. (Sky Sports)
Manchester United inamchunguza beki wa Itali na AC Milan Leonardo Bonucci, 31. (Yahoo)
Aaron Mooy |
Manchester City inatazama uwezekano wa kumsaini
kiungo wa kati wa Australia Aaron Mooy, 27, kutoka Huddersfield . City pia ina
mpango wa dau la £20m huku Everton, West Ham United na Southampton pia
wakipanga kumnunua Mooy. (ESPN)
Divock Origi |
Wolves wamekataa ombi la dau la £12m kwa mshambuliaji wa Fulham na raia wa Ureno Ivan Cavaleiro, 24, (Sky Sports)
Craig Dawson |
West Brom haimtaruhusu beki wa Uingereza Craig Dawson kuondoka katika klabu hiyo kwa gharama ya chini. Klabu hiyo ilikataa dau la £12m kutoka West Ham kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports)
Stoke City wanakaribia kuweka mkataba na winga wa West Brom na Jamhuri ya Ireland James McClean, 29, baada ya kuimarisha dau la kwanza la £4m bid. (Mail)
Marcelo Bielsa |
Sporting Lisbon itamfuta kazi mkufunzi wake Sinisa Mihajlovic, siku chache tu baada ya kuajiriwa.(Record)
0 comments:
Post a Comment