Manchester United wako tayari
kumsaini kipa wa klabu ya Stoke ,35, Lee Grant. Mchezaji huyo wa zamani
wa kikosi cha Uingereza kisichozidi umri wa miaka 21 atatumika kama kipa
wa ziada kwa David de Gea na Sergio Romero. (Telegraph)
Ajenti wa kiungo wa kati wa Napoli Jorginho, 26, anadai kwamba mchezaji huyo anakaribia kukamilisha uhamisho wake hadi Manchester City kwa dau la £43m . (Mirror)
Crystal Palace imempatia kocha Roy Hodgson kandarasi mpya ambayo itamweka katika klabu hiyo hadi 2020. (Sky Sports)
Everton inamnyatia mshambuliaji wa Croatia katika kombe la dunia Ante Rebic. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anaichezea klabu ya Eintracht Frankfurt. (Mirror)
Klabu hiyo pia ina hamu ya kumsajili kipa wa Manchester City Angus Gunn, 22, katika mkataba ambao unaweza kufika dau la £15m. (Mail)
Manchester City haitaangazia kifungu cha ununuzi cha kandarasi ya mchezaji wa Huddersfield raia wa Australia Aaron Mooy , 27 . (Manchester Evening News)Kungo wa kati wa Argentina na West Ham Manuel Lanzini, 25, anasema kuwa anatarajia kupona kutoka katika jeraha lake la goti kufikia mwanzo wa 2019. (Fox Sports)
Liverpool imemsajili mshambuliaji wa Uingereza wa timu ya vijana Bobby Duncan, 17, kutoka Manchester City. Duncan ni binamu wa aliyekuwa kiungo wa kati wa Liverpool Steven Gerrard. (Liverpool Echo)
0 comments:
Post a Comment