Kiungo mshambuliaji Nyota
wa timu ya Taifa ya Brazil, Neymar Junior akipiga mpira kwa kisigino na kumtoka
kiufundi mchezaji wa timu ya Taifa ya Serbia katika mtanange mkali wa mchezo wa
Kundi E Kombe la Dunia uliopigwa 27, Juni 2018, Jumatano Uwanja
wa Otkrytiye Arena mjini Moskow nchini Urusi.
Brazil iliibuka kidedea
kwa kuibamiza Serbia kwa mabao 2-0, mabao ya Paulinho dakika ya 36
na Thiago Silva dakika ya 68, hivyo kuiwezesha kufuzu hatua ya 16 Bora
ambapo itakutana na wapinzani wao wakubwa kutoka amerika ya kusini timu ya
Taifa ya Mexico 2 Julai, 2018.
Timu ya Taifa ya Uswisi
iliyotoa sare ya mabao 2-2 na Costa Rica nayo imefuzu pia hatua ya 16 Bora
na itamenyana na timu ya Taifa ya Sweden 3 Julai,2018.
0 comments:
Post a Comment