Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Yusuph Singo amewataka viongozi wa
mchezo wa kuogelea nchini (TSA) kutorudi nyuma katika malumbano badala
yake wasimamie maelekezo ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Mwakyembe ya kuiboresha katiba ya chama chao na hatimaye
waelekea katika uchaguzi wao mkuu ulioelekezwa kufanyika mapema baada ya
kukamilika kwa katiba.
Maelezo hayo ameyatoa wakati wa kikao cha kuipitia katiba ya chama
cha mchezo wa kuogelea nchini baada ya kuagizwa kufanya hivyo na Mhe.
Waziri mwishoni mwa wiki katika kikao chake na viongozi wa mchezo huo
tarehe 10 Juni, 2018, kikao kilichofanyika jana tarehe 13 June, 2018
katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
“Tusirudi nyuma tulikotoka kwenye malumbano, tumepewa maelekezo na
Waziri, lengo ni kuiboresha katiba hii itakayotusaidia sisi
wote,”alisema Singo.
Rasimu hiyo ya Katiba ya chama cha kuogelea Tanzania imepitiwa
kipengele kimoja baada kingine na wataalam wa Michezo akiwemo Mkurugenzi
huyo wa Michezo Yusuph Singo,Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) Alex Nkenyenge, Kaimu Msajili Ibrahim Mkwawa kwa pamoja na
aliyekuwa Katibu wa TSA Ramadhan Namkoveka na wajumbe wote wa kamati ya
muda iliyoundwa kuandaa rasimu hiyo akiwemo, Mwenyekiti Alexander
Mwaipai, Imani Ahmaya, Amina Mfaume,Inviolata Itatiro na Anna
Shanalingigwa.
Hata hivyo baada kupitiwa kwa kina rasimu katiba hiyo wameteuliwa
wajumbe watatu kuingiza maboresho hayo na kuwapitisha tena wadau wao na
maafisa Michezo walioelekezwa kabla ya kuipeleka kwa Msajili ili
isajiliwe.
Aidha, Singo ameelekeza BMT kutangaza uchaguzi huo mapema wiki ijayo kwakuwa katiba ipo katika hatua za mwisho.
Maboresho ya rasimu ya katiba ya chama cha mchezo wa kuogelea nchini
yamemuhusisha Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Yusuph Singo, Kaimu
Katibu Mkuu wa BMT na Msajili Ibrahim Mkwawa pamoja Katibu wa TSA
Ramadhan Namkoveka na wajumbe wote wa kamati ya muda iliyoundwa kuandaa
rasimu hiyo akiwemo, Mwenyekiti Alexander Mwaipai, Imani Ahmaya, Amina
Mfaume,Inviolata Itatiro na Anna Shanalingigwa.
Home
»
KITAIFA
» MKURUGENZI WA MAENDELEO YA MICHEZO AWATAKA VIONGOZI WA TSA KUTORUDI NYUMA WASIMAMIE MAAGIZO YA WAZIRI.
Thursday, June 14, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment