Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim
Majaliwa Kassim amewapongeza walimu wa michezo nchini kwa kazi nzuri
wanayofanya ya kutumia muda mwingi kuwaandaa wanafunzi kwa kuwapa
utaalam mzuri wa kimichezo ambao kwa sasa wanaonyesha vipaji vyao katika
mashindano ya UMISSETA kitaifa.
Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo tarehe 9 Juni 2018, katika ufunguzi rasmi wa mashindano ya UMISSETA 2018, yenye kauli mbiu “Michezo, Sanaa na Taaluma ni msingi wa maendeleo ya mwanafunzi katika Taifa letu”,ufunguzi uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
“niwapongeze sana walimu wa michezo nchini kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutumia muda mwingi kuwaandaa wanafunzi kwa kuwapa utaalam mzuri wa kimichezo ambao kwa sasa wanaonyesha utaalam walioupata na vipaji vyao katika mashandano haya ya UMISSETA”,alisema Mh. Majaliwa.
Mheshimiwa waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akipuliza filimbi penati ipigwe kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya UMISSETA 2018 jijini Mwanza. |
Aidha mheshimiwa majaliwa ameishukuru kampuni ya chapa ya Coca Cola kwa kudhamini mashindano ya UMISSETA kwa miaka kadhaa sasa, kwani imeweza kuibua vipaji vingi nchini na kulisaidia taifa kuwa na wachezaji mahiri wanaocheza soka la kulipwa ndani na nje ya nchi.
Mh. Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mh. Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza na baadhi ya viongozi wa kampuni ya chapa ya Coca Cola. |
“niishukuru kampuni ya chapa Coca Cola kwa mchango mkubwa waliouonyesha kwa kudhamini mashindano haya kwa miaka kadhaa sasa, kwani yemekuwa ndio chachu kubwa ya kuibua vipaji vingi nchini na kulisaidia taifa kuwa na wachezaji mahiri wanaocheza soka la kulipwa ndani na nje ya nchi”, alisema Mh. Majaliwa.
Mh. Majaliwa akiteta jambo na Mh. Shonza na katibu wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed S. Kiganja ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa maadhimisho ya kitaifa ofisi ya waziri Mkuu. |
Kwa upande wake naibu waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza(mbunge wa viti maalum mkoa wa Songwe),kwa niaba ya mheshimiwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison George Mwakyembe, amemshukuru mheshimiwa waziri mkuu kwa kuona umuhimu wa michezo nchini na kuacha kazi zake na majukumu mengine aliyonayo na kuweza kukubali kuja kufungua mashindano ya UMISSETA 2018.
“mheshimiwa waziri mkuu kwa niaba ya mheshimiwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, nikushukuru sana kwa kuona umuhimu wa michezo nchini na kukubali kuacha kazi zako na majukumu mengine uliyonayo ili uweze kuja kufungua mashindano haya ya UMISSETA 2018 hapa jijini Mwanza”,Alisema Mh. Shonza.
Sanaa nayo haikuachwa nyuma Msanii Abdulaziz Chende almaarufu kama Dogo Janja alipata nafasi ya kutumbuiza katika ufunguzi wa UMISSETA 2018 jijini Mwanza. |
0 comments:
Post a Comment