Akizungumza wakati wa ufunguzi mdogo wa mashindano hayo, mwenyekiti wa michezo hiyo Taifa toka TAMISEMI Leonard Thadeo amesema mikoa itakayobainika kuwatumia wachezaji mamluki itafukuzwa pamoja na viongozi wake sanjari na kusimamishwa kushiriki kwa kipindi cha miaka mitano.
Aidha mwenyekiti huyo ameongeza kuwa hawatakuwa tayari kusimamisha ratiba au kukwamisha michezo hiyo ambayo imechukua muda na gharama kubwa kuandaa lakini pia ni lazima taratibu na kanuni zizingatiwe.
“hatutawavumilia mamluki katika michezo hii, mkoa utakaobainika utafukuzwa pamoja na viongozi wake wakiwamo mwenyekiti, meneja na kocha,” alisema Thadeo.
Nae katibu wa UMISSETA TAIFA 2018, Aaron Sokoni amesema kuwa jumla ya washiriki mwaka huu ni elfu tatu mia nane na tisini na mbili (3892), ikiwa wachezaji ni elfu tatu mia tatu na sitini( 3360) na viongozi ni mia Tano thelathini na mbili (532).
“Tumefungua mashindano ila ufunguzi rasmi utafanyika tarehe 9 Juni, 2018 katika uwanja wa ccm kirumba jijini Mwanza,” alisema Sokoni. |
0 comments:
Post a Comment