Kaimu katibu mkuu ameyasema hayo tarehe 19 Juni, 2018, ofisini kwake alipotembelewa na kiongozi wa maendeleo ya mchezo wa kriketi kanda afrika Bi. Patricia Kambarami akiambatana na katibu wa fedha Kuben Rilvay pamoja na viongozi wa mchezo wa kriketi nchini Taher Kitisa (Mwenyekiti) na Zulfikar Rehemtulla (mtendaji mkuu).
Kaimu katibu mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa maendeleo ya mchezo wa kriketi afrika pamoja na viongozi wa chama cha mchezo wa kriketi Tanzania. |
“ninaamini kuwa Baraza bila vyama vya Michezo lisingekuwepo, hivyo basi vyama vya Michezo vinapaswa kulishirikisha baraza kile kinachoendelea katika chama husika ili kuhakikisha Michezo inafanikiwa katika Nyanja mbalimbali nchini ikiwemo miundombinu, vifaa na mafunzo”,alisema Nkenyenge.
Katika kikao hicho Bi. Patricia amesema wamekuja Tanzania kwa ajili ya kuongelea maendeleo ya mchezo wa kriketi na amekishukuru chama cha mchezo huo kwa kazi nzuri waliyoifanya kuhakikisha kuwa mchezo wa kriketi unafanya vizuri nchini.
“tumekuja Tanzania sio kwa ajili ya chama cha kriketi bali tumekuja kuongelea maendeleo ya mchezo wa kriketi, ila nikishukuru sana chama cha mchezo huu kwa kazi nzuri waliyoifanya kuhakikisha kuwa mchezo wa kriketi unafanya vizuri”, alisema Bi. Patricia.
0 comments:
Post a Comment