Timu ya wavulana ya mpira wa miguu mkoa wa Dar e s saalam imeanza
vyema mashindano ya UMISSETA 2018, kwa kufanikiwa kuichapa timu ya mkoa
wa Lindi kwa mabao 2-0, mabao yaliyopatikana mwishoni kipindi cha kwanza
na mwishoni kipindi cha pili cha mchezo.
|
Timu ya Mkoa wa Dar es salaam ikifunga goli lake la kwanza
katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mkoa wa Lindi uliopigwa katika
uwanja wa shule ya msingi Butimba Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza. |
Timu hiyo imepangwa katika kundi A na timu za mkoa wa Geita, Kigoma,
Kilimanjaro, Lindi, Mbeya na Ruvuma ambapo mpaka sasa timu ya mkoa wa
Mbeya ndio inaongoza kundi hilo baada ya kujikusanyia jumla ya alama
sita baada ya kuzifunga timu ya mkoa wa Lindi kwa bao 1-0 na timu ya
mkoa wa Ruvuma kwa magoli 2-0.
|
Vijana wa Timu ya Dar es salaam wakishangilia moja ya magoli yao waliyofunga katika mchezo wao dhidi ya mkoa wa Lindi. |
Kwa upande wa matokeo mengine timu ya Mkoa wa Lindi iliweza kuitungua
Kigoma kwa magoli 4-1 katika mchezo wake wa kwanza,Geita wakaifunga timu
ya Ruvuma kwa magoli 3-1 na kuifunga tena Kilimanjaro kwa goli 1-0.
Katika kundi B watoto wa makao makuu timu ya mkoa wa Dodoma imefanikiwa
kuifunga timu ya Mkoa wa Simiyu kwa magoli 3-1, huku Pemba wakiifunga
Songwe ambao ndio mabingwa watetezi kwa goli 1-0, sanjari na kuifunga
Shinyanga kwa Goli 1-0.
|
Mchezaji wa Timu ya Mkoa wa Dar es salaam Chris Aweda
akiongoza akiongoza mashambulizi kuelekea katika goli la Lindi, Mchezo
wa kwanza ambao Dar es salaam aliweza kuibuka mshindi kwa kuifunga Lindi
kwa magoli 2-0. |
Katika kundi C mkoa wa Arusha ulifanikiwa kuifunga timu ya Katavi kwa
goli 2-1, huku katika kundi D Morogoro wakitoa suluhu na Manyara kwa
kufungana mabao 1-1, Mara pia wakitoa Suluhu ya bila kufungana na timu
ya Njombe, wakati Mtwara wakikubali kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa timu
ya mkoa wa Unguja na Njombe wakiifunga Kagera kwa goli 1-0.
0 comments:
Post a Comment