Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Mkoa wa Dar es salaam katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa la mashindano ya Copa Coca Cola UMISSETA 2018. |
“niwapongeze sana kampuni ya chapa ya Coca Cola kwa mchango wao mkubwa waliotoa kwa kushirikiana na serikali kufanikisha mashindano ya Mwaka huu,niwaombe msikate tamaa muendelee kudhamini mashindano haya ili vipaji Zaidi viendelee kuibuliwa”,Alisema Mh. Mongela.
Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya Coca Cola Deus Kadico amesema wao kama Kampuni wataendelea kuunga mkono na kufadhili mashindano ya vijana kwa kuwa wanaamini, wanamichezo ni mabalozi wazuri wanaotangaza Taifa letu, vilevile wanao mtazamo wa kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo chipukizi nchini.
“mheshimiwa mgeni rasmi sisi kama kampuni tutaendelea kuunga mkono na kufadhili mashindano ya vijana kwa kuwa tunaamini wanamichezo ni mabalozi wazuri wanaotangaza Taifa letu, lakini pia tunao mtazamo wa kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo chipukizi nchini”, alisema Kadico.
0 comments:
Post a Comment