Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara mjini Evod Mmanda akisoma hotuba ya Mheshimiwa waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo katika uzinduzi wa maandalizi ya UMISSETA 2018 na ugawaji vifaa vya Michezo kwa shule za sekondari, uliofanyika katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
“katika hotuba yake Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI amesema serikali inalojukumu la kuratibu, kusimamia na kuendesha mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini wamejipanga kuhakikisha vipaji vya vijana vinaibuliwa kutoka mashuleni,” Alisema Mmanda.
Aidha katika hatua nyingine Mheshimiwa Mmanda amesema Michezo ni zaidi ya kucheza kwani inatuwezesha kutenda majukumu mbalimbali kwa ushirikiano mwema bila kujali tofauti zozote miongoni mwa wananchi pamoja na kutufundisha ushindani na kutujengea misingi ya kukubali kushinda au kushindwa na kwa matokeo yoyote kuendelea kuwa wamoja.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mjini Mh. Evod Mmanda akipiga penati kuhashiria uzinduzi wa maandalizi ya mashindano ya UMISSETA kwa Mkoa wa Mtwara. |
Ata hivyo Mbali na uzinduzi,Mh. Mmanda alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za sekondari zilizokuwepo kwenye uzinduzi huo,Vifaa ambavyo vimetolewa na kampuni ya Coca-Cola ambayo ni mdhamini mkuu wa mashindano hayo,ambapo mwaka huu imepanga kutoa vifaa vya michezo kwa shule 4,000 za sekondari zilizopo sehemu mbalimbali nchini.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mjini Mh. Evod Mmanda akigawa vifaa kwa moja ya shule itakayoshiriki katika maandalizi ya mashindano ya UMISSETA mwaka 2018 Jijini Mwanza. |
Kwa upande wake Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo,amesema kampuni ya Coca-Cola inajivunia kuwa mdhamini wa mashindano hayo kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo na anaamini vipaji vingi vimeibuliwa na vitaendelea kuibuliwa.
”Udhamini wetu katika mashindano haya tumejikita katika kutoa vifaa vya michezo kwa wachezaji wanaoshiriki kuanzia ngazi ya mkoa hadi ngazi ya taifa,kutoa mafunzo kwa makocha wanaofundisha timu na zawadi kwa timu zinazofanikiwa kufanya vizuri”,alisisitiza Sialouise.
0 comments:
Post a Comment