Katibu Kiganja ameyasema hayo katika uzinduzi wa maandalizi na ugawaji vifaa vya mashindano ya UMISSETA kwa timu za Mkoa wa Tanga, ikiwa ni mwendelezo wa ugawaji vifaa kwa mikoa mbalimbali itakayoshiriki mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA mwaka 2018 jijini Mwanza.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Martin Shigela, amemshukuru Katibu Mkuu wa BMT kwa kusimamamia vizuri Michezo nchini, sanjari na maombi aliyowasilisha kwake kuhusu kuboresha na kuvifufua viwanja vya Michezo mbalimbali katika mji wa Tanga, na kuhaidi kuyatekeleza maombi hayo ili Mkoa uimarishe Michezo na upate nafasi nyingine tena kuweza kuwa wenyeji wa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA.
“Nakushukuru sana Katibu Mkuu wa BMT kwa ushauri mzuri uliotupa,kilichobaki sasa ni kuagiza watendaji wangu kuyatekeleza maombi yako kwani tuna shauku kubwa sana na sisi tuweze kuandaa kwa mara nyingine tena mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA ambayo mara ya mwisho tuliweza kuandaa mwaka 1999 kama ulivyosema,” Alisema Mhe. Shigela.
Ata hivyo Mbali na uzinduzi,Mh. Shigela alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za sekondari zilizokuwepo kwenye uzinduzi huo,Vifaa ambavyo vimetolewa na kampuni ya Coca-Cola ambayo ni mdhamini mkuu wa mashindano haya,ambapo mwaka huu imepanga kutoa vifaa vya michezo kwa shule 4,000 za sekondari zilizopo sehemu mbalimbali nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martin Shigela (aliyemshika mwanafunzi mkono) akigawa vifaa kwa moja ya shule itakayoshiriki katika maandalizi ya mashindano ya UMISSETA mwaka 2018 Jijini Mwanza. |
Mheshimiwa Shigela alisema kampuni ya Coca-Cola kwa kudhamini mashindano hayo kutafanikisha jitihada za kuendelea kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi wa michezo ya soka,mpira wa kikapu na pia kupitia mashindano haya kutaibuliwa vipaji vya wanariadha watakaotamba katika kipindi cha miaka ijayo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martin Shigela akipiga penati kuhashiria uzinduzi wa maandalizi ya mashindano ya UMISSETA kwa Mkoa wa Tanga |
Naye Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo,amesisitiza kuwa kampuni ya Coca-Cola inajivunia kuwa mdhamini wa mashindano haya kwa kipindi cha miaka 3 mfulilizo na anaamini vipaji vingi vimeibuliwa na vitaendelea kuibuliwa.
“Udhamini wetu katika mashindano haya tumejikita katika kutoa vifaa vya michezo kwa wachezaji wanaoshiriki kuanzia ngazi ya mkoa hadi ngazi ya Taifa,”Alisisitiza Sialouise.
0 comments:
Post a Comment