Waziri Mwakyembe amesema ujumbe wa FIFA unajumuisha watu 70, tayari baadhi ya ujumbe huo unaanza kuwasili leo tarehe 19 Februari 2018, na Rais wa FIFA atawasili tarehe 21 Februari usiku na kufikia katika hotel ya Kilimanjaro Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini alichokuwa anazungumza mheshimiwa waziri kuhusu ujio wa FIFA |
Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidau akielezea ajenda za Kikao cha FIFA kitakachofanyika nchini Februari 22, 2018 |
Kwa upande wake katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF Wilfred Kidau, amesema miongoni mwa ajenda kubwa za mwaka huu katika shirikisho la soka Duniani FIFA ni pamoja na kuongelea soka la wanawake Duniani, ya pili ni kuhusu soka la Vijana sanjari na Mradi wa FIFA wa kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya soka kama vile kujenga hostel za wachezaji vijana katika mataifa mbalimbali duniani n.k.
“Mheshimiwa waziri miongoni wa ajenda kubwa za FIFA katika kikao chao mwaka huu ni pamoja na kuongelea soka la wanawake Duniani, ya pili ni kuhusu soka la vijana Sanjari na Mradi wa FIFA wa kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya soka kama vile kujenga hostel za wachezaji vijana katika mataifa mbalimbali duniani n.k.
0 comments:
Post a Comment