Monday, February 12, 2018

Washambuliaji wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba wakishangilia goli la Kwanza lililofungwa na Said Hamis Ndemla
Hatimaye klabu ya Simba  imeanza vyema michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Gendarmarie Tnare kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kiungo Said Ndemla ndiye aliyeanza kuwainua mashabiki wake dakika ya kwanza tu baada ya kufunga kwa shuti la kiufundi la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20, kufuatia Bocco kuchezewa rafu.

Bocco akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 32 kwa kichwa, akitumia mwanya wa kipa wa GendarmerieTnare kuanguka katika harakati za kuokoa.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Azam FC, akarudi tena nyavuni na kufunga bao la tatu dakika ya 45 kwa kichwa tena akimalizia pasi nzuri ya mshambuliaji mwenza, Mganda Emmanuel Okwi.

Kipindi cha pili, Simba inayofundishwa na kocha Mfaransa, Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mtunisia, Mohamed Aymen Hbibi, Mrundi, Masoud Juma na mzalendo, Muharami Mohamed ‘Shilton’ kocha wa makipa haikuwa na makali iliyoanza nayo.

Na dakika ya 50 Gendarmerie wakapoteza nafasi nzuri ya kupata bao la ugenini baada ya mkwaju wa penalti uliopigwa na Moustapha Moussa kufuatia Abdorahim Mohamed kuangushwa kwenye boksi na kiungo Mghana, James Kotei kuokolewa na kipa namba moja Tanzania, Aishi Manula.

Na baada ya mchezo kupooza kwa takriban nusu saa, Mganda Okwi aliyepoteza nafasi nyingi za kufunga katika mchezo huo, akasahihisha makosa yake kwa kufunga bao la nne dakika ya 90 baada ya kuanzishiwa pasi ya pigo la adhabu ndogo na beki anayemudu kucheza kama kiungo pia, Erasto Nyoni.

 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video