Klabu ya Arsenal
ina hamu ya kumsajili mshambuliaji huyo kwa dau la £60m, ambapo Siku ya
Alhamisi , Wenger alisema kuwa Aubameyang ataifaa sana Arsenal , matamshi
ambayo hayakuifurahisha klabu ya Dortmund.
''Tunahisi
kwamba ni kukosa heshima kwa Wenger kuzungumzia kuhusu wachezaji wa klabu nyingine
hatujawasiliana na Arsenal'', alisema Zorc.
Aubameyang
ameadhibiwa mara mbili kwa utovu wa nidhamu msimu huu na alikosa mechi ya
Jumapili ya sare ya 0-0 dhidi ya Wolfsburg baada ya kukosa kuhudhuria mkutano
wa timu.
Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 28 ni mfungaji wa mabao mengi katika timu hiyo msimu huu
baada ya kufunga mabao 13 katika mechi 15.
Dortmund ni ya
nne katika ligi ya Bundesliga, wakiwa na alama 15 nyuma ya viongozi wa ligi
Bayern Munich.
0 comments:
Post a Comment