Klabu ya Everton imekamilisha usajili wa
mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot katika mkataba ulio na thamani ya
£20m katika kandarasi ya miaka mitatu na nusu.
Hatua hiyo inakamilisha huduma za Walcot za miaka 12 katika klabu hiyo ambapo alifunga magoli 108 katika mechi 397
Klabu ya zamani ya Walcott Southampton pia walikuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo.
- Wenger: Nisingeweza kumuuza Walcott
- Wilshere na Walcott wanataka Wenger ajikune kichwa
- Wenger hataki kuzungumzia hatma yake ndani ya Arsenal
''Nilihisi kwamba ni wakati nilifaa kuondoka, ni uchungu lakini ni vyema na nataka kuimarisha mchezo wangu na kuisaidia Everton kushinda mataji kama ilivyokuwa awali'', alisema Walcott.
''Nilizungumza naye na nilihisi hasira aliyokuwa nayo na kile alichotaka kutoka kwangu''.
Katika taarifa yake , Arsenal ilisema: Sote tunamshukuru Walcott kwa mchango wake kwa Arsenal na tunamtakia kila la kheri.
0 comments:
Post a Comment