Klabu hiyo ipo mbioni na pauni milioni 53 kibindoni kuhakikisha kuwa wanampata Aubameyang mwenye umri wa miaka 28. (Mail)
Nayo klabu ya Chelsea pia imejiunga katika mbio za kumpata Sanchez lakini United wana uhakika kuwa kupitia mchezaji Henrikh Mkhitaryan mwenye umri wa miaka 28, kama sehemu ya makubaliano inawaweka katika nafasi nzuri. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo, mwenye umiri wa miaka 32, anataka kurudi Manchester United. (As.com - in Spanish)
Kiungo wa kati wa klabu ya Liverpool raia wa Ujerumani Emre Can, 24, amesema kuwa hajasaini makubaliano ya kujiunga na Juventus msimu huu na bado anazungumza na Liverpool kuhusu kuendelea kubaki katika dimba la Anfield. (Times - subscription required)
Swansea City wamefanya mazungumzo na Atletico Madrid kuhusu makubaliano ya kuwaleta mshambuliaji raia wa Ufaransa Kevin Gameiro mwenye umri wa miaka 30, na mBrazil Nicolas Gaitan mwenye umri wa miaka 29, huko Kusini Wales Januari hii. (Wales Online)
Everton wanajaribu kukamilisha makubaliano ya pauni milioni 20 kwa wing'a wa Arsenal na Uingereza Theo Walcott mwenye umri wa miaka 28, wiki hii. (Mirror)
Meneja wa timu ya Taifa ya Wales Ryan Giggs anatathmini hatua ya kumfanya mchezaji mwenza waliokuwa wanakipiga wote katika klabu ya Manchester United Paul Scholes kuwa mmoja wa kikosi chake. (Mail)
Mtaalamu wa masuala ya kandanda mfaransa Julien Lauren ana uhakika kuwa mshambuliaji wa PSG mBrazil Neymar mwenye umri wa miaka 25, na mchezaji aliye kwenye mkopo raia wa Ufaransa Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 19, wakati mmoja watakuwa wachezaji wa Real Madrid. (BBC Radio 5 live)
Arsenal ilifanya mazungumzo na mshambuliaji wa Bordeaux Malcom siku ya Jumapili na wanatarajia kulipa pauni milioni 40 kwa mBrazil huyo wa miaka 20. (Guardian)
Arsenal na Chelsea wanammezea mate mshambuliaji wa Watford raia wa Brazil Richarlison mwenye umri wa miaka 20. (Sun)
0 comments:
Post a Comment