Sekretarieti
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati
ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
Viongozi
walioshtakiwa kwenye Kamati ya Maadili ni msimamizi wa Kituo cha Mtwara
Dunstan Mkundi, Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Mtwara Kizito Mbano,
Muhasibu msaidizi wa klabu ya Simba Suleiman Kahumbu na Katibu msaidizi
wa Klabu ya Ndanda FC ya Mtwara Selemani Kachele.
Sekretarieti
inawashtaki viongozi hao kwa makosa ya kughushi pamoja na udanganyifu
wa mapato kwenye mchezo namba 94 kati ya Ndanda FC ya Mtwara dhidi ya
Simba ya Dar es Salaam iliyochezwa Disemba 30, 2017 kwenye Uwanja wa
Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Kwa tuhuma hizo viongozi hao watatakiwa kufika mbele ya kamati Januari 18, 2018.
Kamati
ya maadili iko chini ya mwenyekiti Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu
Mwenyekiti Wakili Steven Zangira, Wajumbe ni Glorious Luoga, Walter
Lungu na Amin Bakhresa
0 comments:
Post a Comment