Meneja wa klabu
ya Everton inayoshiriki ligi kuu soka nchini Uingereza Sam Allardyce amesema Beki kisiki wa klabu
hiyo Seamus Coleman, amerejea kikosini na kuendelea kujifua baada ya kukaa nje tangu mwaka jana akiuguza
jeraha la mguu alilolipata akiwa na timu yake ya Taifa ya Ireland.
Allardyce alisema Coleman alicheza mchezo wake wa mwisho wa kufuzu Kombe la Dunia akiwa na timu ya Ireland dhidi ya Wales mwezi Machi mwaka 2017, ndipo alipopata jeraha ambalo limemuweka nje mpaka hivi sasa.
"Seamus Coleman anastahili kurudi kucheza katika nafasi yake,tunashukuru ameanza mazoezi polepole kwa matumaini kuwa ataendelea vizuri na kupona kabisa jeraha hilo ili aweze kukisaidia kikosi cha Everton ambacho kwa sasa tunapambana tumalize katika nafasi nzuri msimamo wa ligi kuu soka uingereza," alisema Allardyce.
0 comments:
Post a Comment