MAN U KUMBE INAWEZEKANA KUIKAMATA MAN CITY
Klabu ya Manchester United ilichukua muda wa kuifuata Arsenal ili kuhakikisha wanaipata sahihi ya mshambuliaji wa klabu hiyo Alexis Sanchez huku hapo jana wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stoke city mtanange uliochezwa katika uwanja wa Old Trafford.
Antonio Valencia na Anthony Martial waliweza kufumania nyavu katika nusu ya kwanza, na mshamuliaji Romelu Lukaku akirudi kambani baada ya mapumziko, hii inakuwa ni mara ya nne mfululizo kwa klabu ya manchester united kuweza kuibuka na ushindi mbele ya klabu ya Stoke City.
Lakini licha ya kikosi cha Manchester united kuonekana kipo katika kiwango cha juu katika siku za hivi karibuni bado klabu hiyo inauitaji wa kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ikiongozwa na makinda kama vile Jesse Lingard, antonial martial pamoja na marcos rashford bila kumsahau mbeligiji Lukaku, kocha wa klabu hiyo raia wa Ureno Jose Mourihno amesema kuwa bado klabu inamuitaji Alex Sanches na endapo kama watafanikiwa kumsajili mchezaji huyo basi atakuwa na msaada mkubwa sana katika kikosi hicho.
"Ni wazi tunaiona Manchester City mbele yetu wakiwa wametuacha kwa alama kumi na mbili katika msimamo wa ligi baada ya kupoteza dhidi ya Liverpool, nina washambuliaji wazuri ambao wanaumri mdogo kwa mfano Jesse Lingard, Antonial Martial, Marcus Rashford pamoja na Lukaku lakini bado tunaitaji Huduma ya Alex Sanchez na endapo kama atajiunga na sisi basi ataisaidia klabu na kuiongezea nguvu na kufanya vizuri," Alisema Jose Mourihno.
0 comments:
Post a Comment