Kocha wa Klabu ya Manchester United Jose Mourinho |
Klabu ya Manchester United inakaribia kufikia makubaliano na kocha wake Jose Mourinho wa kuongeza mkataba mpya.
Taarifa za ndani ya klabu zinaeleza kuwa kama kocha huyo atasaini mkataba mpya utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2021.
Licha ya kulaumiwa na wachambuzi wengi wa soka pamoja na washabiki wa klabu ya Man United kuwa timu hiyo inacheza mchezo wa kujilinda bado viongozi wa United wanaona kuwa Mourinho anaweza ibeba timu hiyo katika kuipa mataji makubwa barani Ulaya.
Mourinho alijiunga na United mwaka 2016 kuchukua mikoba ya Luis Van Gaal, ameisadia Man United kutwaa ubingwa mwa kombe la Europa na Lile la EfL Carabao.
0 comments:
Post a Comment