Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya
Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Macron wenye thamani ya
Sh. Bilioni 2 kwa ajili ya utengenezaji na uuzaji wa jezi za klabu hiyo.
Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo katika makao makuu ya klabu yaliyopo makutano ya mitaa ya twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniphace Mkwasa “MASTER” amesema mkataba huo utakuwa na ongezeko kutokana na makubaliano waliyofikia. Kwa mujibu wa Mkwasa ni kwamba dau litakuwa likiongezeka kulinganana idadi ya mauzo ya jezi za mashabiki.
Ikumbukwe kuwa Desemba mwaka Jana 2017, Macron walisaini mkataba na miaka miwili na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa udhamini wa jezi wa timu zote za taifa zikiwemo za vijana na wakubwa kwa wanawake na wanaume wenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 800.
Katika hatua nyingine, Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten
amesema kikosi kipo tayari kwa mchezo wa Leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara dhidi ya Mwadui FC utakaoanza majira ya Saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Ten amesema katika mchezo wa leo klabu
itaendelea kuwakosa Wazimbabwe, kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donald
Ngoma ambao ni majeruhi pamoja na Geofrey Mwashiuya, wakati Mzambia Obrey
Chirwa akitumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu hadi sasa akiwa amekwishakosa
mechi moja.
"Tunawachezaji
wetu ambao bado ni wagonjwa kuna Ngoma, Mwashiuya na Kamusoko wataukosa mchezo
wa Leo dhidi ya Mwadui pamoja na Chirwa ambaye anaitumikia adhabu iliyotolewa
na Kamati ya Maadili,” alisema Dismas Ten.
Kuhusu, Mrundi Amissi Tambwe aliyekuwa anasumbuliwa na Malaria, Dismas amesema kwamba amepona, lakini kujumuishwa kwenye mchezo wa Leo ni mipango ya mwalimu.
0 comments:
Post a Comment