Licha
ya Ronadinho kutocheza soka la kiushindani toka mwaka 2015 amekua akicheza
michezo ya mabonanza mbalimbali ambapo Kaka
na wakala wa mchezaji huyo Roberto Assis amethibitisha kuwa umefika mwisho kwa
fundi huyo wa kibrazil kucheza soka.
Ronaldinho
alianzia soka lake katika klabu ya Gremio ya nchini kwao Brazil kabla ya kujiunga na
Paris St-Germain mwaka 2001 na baadae kujiunga na Barcelona alikong'ara sana kwa kusakata kabumbu safi na chenga za maudhi.
Katika
msimu wa 2010 -2011 alijiunga na Ac Milan ya Italia kabla ya kurudi kwao na
kujiunga na Flamengo mwaka 2011. Kisha alichezea vilabu vya Atletico Mineiro,
na Queretaro ya nchini Mexico na kurudi tena kwao Brazil katika klabu ya
Fluminense.
0 comments:
Post a Comment