Afisa Habari wa Baraza la Michezo la Taifa Bi Najaha Bakari akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Uchaguzi wa wa Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT |
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa BMT Bi Najaha Bakari amesema fomu zimeanza kutolewa katika ofisi za BMT zilizopo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kupatikana katika tovuti ya Baraza ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz, kwenye ofisi za viongozi wa ngumi za Ridhaa mikoani na ofisi za BFT kuanzia Tarehe 17 Januari hadi 15 Februari mwaka 2018.
Aidha, usaili utafanyika Tarehe 23 Februari siku ya Ijumaa kabla ya kuelekea katika uchaguzi huo Tarehe 24 Februari siku ya Jumamosi.
Nafasi zinazogombewa ni;
Nafasi ADA
- Rais 200,000/=
- Makamu wa Rais 150,000/=
- Katibu Mkuu 150,000/=
- Mweka Hazina 150,000/=
- Wajumbe 9 50,000/=
Hairuhusiwi kugombea nafasi yoyote kama wewe ni Mchezaji.
- Mgombea anatakiwa awe na umri husiopungua miaka 25
- Hasiwe ametenda kosa lolote la Jinai
- Awe na Elimu ya Kidato cha nne na kuendelea.
- Katika nafasi ya Mweka Hazina mgombea lazima awe na cheti cha Uhasibu
- Wajumbe wanaogombea nafasi hiyo lazima wawe na uzoefu na ngumi za Ridhaa.
Malipo ya fomu yanafanyika katika akaunti ya Baraza kwa jina la National Sports Council Ac.No. 20401100013-Bank ya NMB na kuwasilisha Baraza fomu iliyojazwa pamoja na risiti iliyolipiwa Benki.
0 comments:
Post a Comment