Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja akizungumza kuhusu Msiba wa Athumani Juma Chama |
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
Ndugu Mohammed Kiganja amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha
mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Athuman Juma
“Chama” maarufu kama Jogoo aliyefariki usiku wa kuamkia Januari 8, 2018 kwenye
hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika salamu hizo za rambirambi Katibu Kiganja
amesema ni Pigo kubwa sana kumpoteza mchezaji huyo wa zamani, na kutoa pole kwa
familia,ndugu jamaa na marafiki.
BMT linatoa rambirambi kwa familia ya marehemu
kutokana na msiba huo.
“Ni masikitiko makubwa kumpoteza Chama ambaye
alilitumikia taifa naungana kumuombea marehemu na ninatoa pole kwa familia
yake,wanafamilia wa mpira wa miguu ,ndugu na jamaa pamoja na marafiki,Mungu
aiweke mahala pema peponi roho ya Marehemu Athuman Juma Chama, Amina.
Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars, Klabu ya Yanga na Pamba Athumani Juma Chama akiwa katika moja ya mechi alizocheza kipindi hicho. |
Marehemu Chama katika enzi ya uhai wake pamoja na
kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars,pia ameshawahi kukipiga katika
klabu ya Yanga akitokea klabu ya Pamba ya Jijini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment