Miamba ya soka nchini Uingereza klabu ya Manchester United imeonekana ina nafasi nzuri sana ya kumnunua kiungo mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Alexis Sanchez baada ya klabu ya Manchester City kutangaza kujitoa katika kinyang'anyiro cha kumuwania mchezaji huyo raia wa chile.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alisema Jumapili kwamba mustakabali wa Sanchez utaamuliwa katika kipindi cha saa 48 zijazo baada ya kumuacha mchezaji huyo nje ya kikosi kilichocheza mechi ya ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Bournemouth na Arsenal kupoteza mchezo huo kwa kukubali kipigo cha magoli mawili kwa moja.
Sanchez alitaka sana kwenda kujiunga na vinara wa ligi kuu nchini Uingereza kwa sasa klabu ya Manchester City lakini maasimu wao United wako tayari kutimiza matakwa ya mchezaji huyo na klabu ili kuweka urahisi wa klabu hiyo kumsajili mchezaji huyo.
Mkataba wa Sanchez unafikia kikomo mwisho wa msimu huu ambapo katika dirisha la usajili majira ya joto mwaka jana alikaribia kujiunga na City kwa ada ya £60 milioni, lakini uhamisho wake ukatibuka baada ya Arsenal kushindwa kumnunua kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Thomas Lemar.
0 comments:
Post a Comment