Na Zaka Zakazi, Dar es Salaam
Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, msimu uliopita ilikumbwa na kishindo baada ya ingizo jipya, RB Leipzig kufanya kisichotarajiwa.
Timu hiyo ya kimaajabu tangu kuanzishwa kwake mpaka mfumo wake wa uendeshwaji, ilicheza msimu wake wa kwanza wa Bundesliga na kumaliza nafasi ya pili, nyuma ya wababe Bayern Muninch huku ikiishangaza Borussia Dortmund iliyoshika nafasi ya tatu.
Nyuma ya mafanikio ya timu hiyo yupo mshambuliaji Yussuf Poulsen. Nyota huyu ambaye ni nusu mtanzania na nusu mdanish, ametoa mchango mkubwa msimu huu, alijiunga na timu hiyo mwaka 2013 ikiwa daraja la tatu.
Poulsen ni mtoto wa baharia wa kidigo kutoka Tanga Tanzania, aliyezamia Denmark na kuoa huko. Alifariki kwa maradhi ya saratani na kumuacha mwanaye akiwa na umri wa miaka 6.
Poulsen anajivunia kuwa na asili ya Tanzania kama ambavyo alionekana kwenye picha(kushoto) akiwa kajichora bendera ya Tanzania na ya Denmark kuonesha kwamba nchi zote mbili zinamhusu.
Hivi sasa ligi zikiwa ziko mapumziko barani Ulaya, Yussuf amekuja kwenye ardhi ya asili yake, Tanga Tanzania na kujichanganya na wadigo wenzake(picha ya kulia)...japo wasambaa nao wanaruhusiwa. Na wengine pia!
0 comments:
Post a Comment