Sunday, January 29, 2017


LIGI kuu soka Tanzania Bara imeendeleo leo kwa mechi mbili kuchezwa katika Miji Miwili Tofauti.
Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Mabingwa Watetezi Yanga SC wamerejea kileleni mwa msimamo wa VPL baada ya kuwafunga Mwadui FC mabao 2-0.
Mabao yote mawili ya Yanga yamepachikwa wavuni na Obrey Chola Chirwa ambaye sasa amefikisha mabao 7 msimu huu kwenye mechi za Ligi kuu.
Yanga wamewashusha kileleni mwa Msimamo mahasimu wao Simba ambao jana walifungwa 1-0 na Azam FC.
Simba sasa wanashika nafasi ya pili kwa pointi 45, huku Wajangwani wakibarizi kileleni kwa pointi 46 na timu zote zimecheza mechi 20.
Mkoani Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Wenyeji Ndanda FC wamepoteza mechi kwa  kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Wanalizombe Majimaji FC.
Bao pekee la Majimaji limefungwa na Kelvin Sabato Kongwe 'Kiduku'.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video