VINARA wa Ligi kuu soka nchini Hispania, La Liga, Real Madrid, usiku wa kuamkia leo wamechomoza na ushindi wa 3-0 dhidi ya Real Sociedad kwenye mechi ya La Liga iliyochezwa Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Kama kawaida, Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo alifunga goli na kutoa pasi moja ya goli.

Dakika ya 38' kipindi cha kwanza, Mateo Kovacic alimazilia pasi ya Ronaldo na kuipachikia bao la kuongoza Real Madrid.

Naye Ronaldo dakika ya 51' alitengenezewa pasi nzuri na Kovacic ambapo aliimalizia vizuri akiifungia Real Madrid bao la pili.

Alvaro Morata alihitimisha safari ya mabao dakika ya 82' akifunga bao la tatu kufuatia pasi nzuri ya Lucas Vazquez.
Kwa matokeo hayo, Real Madrid wanazidi kujikita kileleni kwa pointi 46 walizovuna kwenye mechi 19, huku mahasimu wao Barcelona wakishika nafasi ya tatu kwa pointi 42 baada ya kucheza mechi 20.
MATOKEO YA MECHI ZA JANA LA LIGA
ANGALIA MSIMAMO WA TANO BORA LA LIGA HAPO CHINI
0 comments:
Post a Comment