TIMU ya Taifa ya kandanda ya Ghana, Black Stars, imetinga nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Africa, AFCON 2017, baada ya kuichapa mabao 2-1 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo wa robo fainali uliopigwa usiku huu.
Mabao ya Ghana yamefungwa na ndugu wawili, Jordan Ayew kwa shuti kali na Andrew Ayew aliyepachika kwa mkwaju wa penati.
Bao la kufutia machozi kwa Congo DR limewekwa wavuni na Paul Jose Mpoku kwa kombora kali la Mtindo wa 'Mama Mkanye Mwanao'.
Ghana inaungana na nchi za Burkina Faso, Cameroon kwenda nusu fainali, wakati mchezo wa mwisho wa Robo fainali unapigwa usiku huu kati ya Misri na Morocco na timu moja itakamilisha idadi ya timu nne za kwenda Nusu Fainali.
0 comments:
Post a Comment