Pamoja na kuifunga Simba, kipa aliyefanya maajabu kwa kuokoa michomo kadhaa ya washambulizi wa Simba, Aishi Manula amesema bado hawajakaa vizuri katika ligi.
Manula amesema ushindi wao wa bao 1-0 dhidi Simba ni changamoto kwao waendelee kufanya vema ili kurejea katika nafasi za juu kwenye Ligi Kuu Bara.
"Ushindi ni jambo zuri kabisa, lakini tunatakiwa kujitahidi na kufanya vizuri zaidi ya hapa kwa kuwa kwenye ligi kuu hatuko vizuri kwa kweli," alisema.
Manula alikuwa kizingiti kikubwa kwa Simba kuhakikisha inapata ushindi au kusawazisha baada ya kupangua michomo kadhaa iliyoonekana kuwa ingeipatia Simba bao.
Simba imepoteza mechi yake ya kwanza katika mzunguko wa pili kwa kuchapwa bao 1-0 na Azam FC ikiwa imefunga Simba mara mbili mfululizo ndani ya wiki mbili. Mara ya kwanza ilikuwa mjini Zanzibar kwenye fainali Kombe la Mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment