Mabingwa watetezi wa kombe la FC, Manchester United wameibuka na ushindi mnono wa mabao manne kwa bila dhidi ya Wigan Athletic na kutinga raundi ya tano ya kombe hilo, huku stori kubwa ikiwa ni Bastian Schweinsteiger kuwa kwenye orodha ya wachezaji wanne waliofunga magoli.

Dhahama ilianza dakika ya 44 kwa Marouane Fellaini kuifungia Man United bao la kuongoza, baadaye dakika ya 57, Chris Smalling akaandika la pili, dakika ya 74' Mkhitaryan akapachika la tatu na dakika ya 81, Bastian Schweinsteiger.

Mbali na kufunga, Mjerumani huyo ambaye hana nafasi kwenye kikosi cha Man United, alitoa pasi ya goli la kwanza na alipofunga goli lake, mashabiki wa Manchester United waliofurika Old Trafford walimshangilia na kumpa heshima kubwa.

Hata kocha wa Man United, Jose Mourinho ambaye huwa anampanga mara chache mno kiungo huyo mkongwe, alionekana mwenye tabasamu kubwa akifurahia urejeo huo wa Schweinsteiger.
Kabla
Mechi hiyo ya Man United na Wigan kuanza, Kepteni Wayne Rooney
alitunukiwa Kiatu cha Dhahabu na Klabu yake baada ya kuvunja Rekodi ya
Ufungaji Bora wa Klabu hiyo na aliemkabidhi ni Sir Bobby Charlton ambae
alikuwa akishikilia Rekodi hiyo kwa Miaka 44.
Ukiondoa
Sare ya Mechi ya Kwanza kabisa ya Raundi ya 4 ambapo Derby County na
Leicester City zilifungana 2-2 na sasa zitarudiana huko King Power
Stadium Nyumbani kwa Leicester, Mechi zote nyingine zilitoa Washindi 15
na sasa zimesonga Raundi ya 5 na Timu zitajua Wapinzani wao wa Raundi ya
5 Jumatatu Usiku wakati Droo itakapofanyika.
Mechi za Raundi ya 5 zitachezwa kati ya Ijumaa Februari 17 na Jumatatu Februari 20.
0 comments:
Post a Comment