Thursday, January 12, 2017

Wakati timu pinzani ‘derby’ za JKT Ruvu na Ruvu Shooting zikitarajiwa kuchuana kesho Ijumaa Januari 13, 2017 kwenye Uwanja wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Bodi ya Ligi Kuu, imetangaza tarehe rasmi za michezo mitatu ambayo awali haikupangiwa tarehe katika ratiba.
Mbali ya ‘derby’ ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting, Jumamosi Januari 14, 2017 kutakuwa na mchezo mwingine wa upinzani kati ya Stand United na Mwadui FC – zote za Shinyanga na zitapambana kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.
Kadhalika siku hiyo ya Jumamosi Januari 14, 2017 Kagera Sugar itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika mchezo mwingine wa VPL.
Jumapili Januari 15, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu ya Vodacom ambako Mbao itakuwa mwenyeji wa African Lyon ya Mwanza katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kadhalika Jumatatu Januari 16, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu ambako Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Michezo mitatu ambayo haikupangiwa tarehe hapo awali kwa alama ya TBA ikiwa na maana ya kutajwa baadaye (To Be Announced), tayari Bodi ya Ligi – chombo cha Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), kinachosimamia na kuendesha ligi, imepanga tarahe.
Tarehe hizo ni Januari 17, 2017 – siku ya Jumanne kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Majimaji itakayowaalika mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Young Africans ya Dar es Salaam katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kadhalika mechi nyingine ziliopangiwa tarehe na muda ni kati ya Mtibwa Sugar itakayocheza na Simba, Jumatano Januari 18, 2017 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mchezo huu wa Azam na Mbeya City utaanza saa 1.00 usiku wakati michezo yote tajwa hapo juu itaanza saa 10.00 jioni lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa mashabiki kushuhudia mechi nyingi kupitia Kituo cha Televisheni cha Azam - Wadhamini wenza wa ligi hiyo.
Ligi hiyo ambayo pia inabarikiwa na Benki ya Diamond Trust (DTB), Mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom iliyokuza ubora wa huduma zake hapa nchini katika mawasiliano ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na intaneti yenye kasi.
..…………………………………………………………………………..............
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video