Uongozi wa
Ndanda fc kutoka mkoani Mtwara imethibitisha kumalizana na Kocha Abdallah
Mohamed Bares na nafasi yake itakaimiwa na Mkurugenzi wao wa Ufundi Hamim
Mawazo mpaka pale msimu wa 2016/2017 wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Mwezi Oktoba
mwaka huu baada ya kuipa ubingwa wa Ligi kuu ya visiwani Zanzibar Timu ya
Zimamoto, Kocha huyo alitambulishwa rasmi huko mkoani Mtwara kuwa ni Kocha mpya
Ndanda lakini tangu kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa VPL kocha huyo
hakuonekana tena kwa wana kuchele.
Hii si mara
ya kwanza kwa Ndanda fc kumtambulisha Kocha mpya ambae haichukui hata miezi
sita kabla ya kutemana nae jambo linalotiliwa shaka kuwa huenda suala la
mikataba ikawa ni kikwazo kwa timu ya Ndanda.
0 comments:
Post a Comment