Sam Allardyce huenda akarithi mikoba ya Alan Pardew kuifundisha klabu ya Crystal Palace.
Pardew aliyekuwa kocha wa Palace alifutwa kazi jana na atapewa fidia ya kuvunjiwa mkataba ya pauni milioni 3.
Kama Allardyce hatabadili upepo, anatarajiwa kuwa kocha ajaye wa Palace.

Kocha huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Soka ya England, amekuwa kwenye rada za Palace kwa mwezi mmoja zaidi na hii ilitokana na kampeni mbaya ya Pardew katika mechi za Ligi kuu ya England-EPL.
0 comments:
Post a Comment