Monday, December 26, 2016

Wachezaji wa Yanga, jana Jumapili wamekumbana na balaa katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ya kujiandaa na mchezo wao wa Jumatano dhidi ya Ndanda FC.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Mzambia, George Lwandamina alitumia takribani saa mbili na nusu kuwahenyesha wachezaji hao ambao hivi karibuni kabla ya kupambana na African Lyon walifanya mgomo wa siku mbili bila ya kufanya mazoezi wakiushinikiza uongozi wao kuwalipa mshahara wao wa mwezi Novemba pamoja na posho zao walizokuwa wakidai.

Mazoezi hayo ya jana yalianza majira ya saa 2:00 asubuhi hadi saa 4:30.

Katika mazoezi hayo Lwandamina alitumia muda mwingi kuwakimbiza kuliko kucheza mpira, jambo lililowafanya baadhi yao baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo kuondoka uwanjani hapo wakiwa wamechoka kupita maelezo.

Hata hivyo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Juma Mwambusi aliliambia Championi Jumatatu kuwa lengo kubwa la mazoezi hayo lilikuwa ni kuhakikisha wachezaji hao wanarejea kwenye hali yao ya kawaida waliyokuwa nayo hapo awali.
“Tunajitahidi kuhakikisha wachezaji wanarudi katika hali yao ya kawaida kwani kabla ya mechi yetu ya na African Lyon hawakufanya mazoezi kwa muda wa siku mbili.

“Hivyo tunataka wawe fiti tayari kwa mechi yetu ya Jumatano dhidi ya Ndanda FC ambayo tunataka tupate matokeo mazuri yatakayoturudisha katika harakati zetu za kutetea ubingwa wetu,” alisema Mwambusi.

Yanga hivi sasa inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 37 ambapo timu ya Simba ndiyo inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 41.

SOURCE: CHAMPIONI

26 Dec 2016

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video