KOCHA Mkuu wa Mbeya City Fc, Maarufu 'Wanakoma Kumwanya' Kinnah Phiri amesema ameajindaa
vizuri ‘kuikabili’ Young Africans kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Tanzania bara uliopangwa kuchezwa leo Jumatano Uwanja wa
Sokoine Jijini Mbeya.
Kocha Phiri ameiambia mbeyacityfc.com kuwa
anaamini utakuwa mchezo mzuri na mgumu kwa sababu timu zote mbili
zimetoka kushinda mechi zake zilizopita huku akiahidi ‘kuiduwaza’ Yanga
kwa kipigo kutokana na maandalizi mazuri aliyoyafanya kwa kikosi chache
na kutupilia mbali hofu yoyote kutoka kwa timu hiyo akiamaini timu zote
hizi mbili zina mchezo sawa.
“Kweli,kesho (leo) tunacheza na Yanga, utakuwa mchezo mzuri kwa
sababu timu zote zimeshinda michezo iliyopita,sisi tumejiandaa vizuri
kuhakikisha tunashinda,hatuna shaka yoyote kwa sababu timu zote zina
mchezo sawa, jambo jema ni maandalizi tuliyoyafanya na sapoti ambayo
tutaipata kutoka kwa mashabiki wetu,watu waje uwanjani na wajiandae
kushangaa kile kitakachofanywa na timu yangu”alisema.
Akiendelea zaidi kocha huyo raia wa Malawi alisema kuwa City
imebakiza michezo miwili, wa kesho na ule wa tarehe 7 dhidi ya Mtibwa
Sugar utakaochezwa Manungu Turiani hivyo anachokitizama sasa ni
kushinda michezo hii miwili ili kuweza kupata pointi 6 ambazo zitaicha
timu City kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi kabla ya kukamilika
kwa duru ya kwanza.
“Tumebakiwa na michezo miwili, wa kesho na ule ambao
tucheza dhidi ya Mtibwa, tuko kwenye nafasi ya tisa sasa, lengo letu ni
kushinda michezo hii ilikuweka mazingira mazuri katika msimamo wa ligi
kabla hatujamaliza duru ya kwanza, hii ina maana kuwa tutakapo rejea
kuanza duru ya pili tutacheza kwa nguvu kutafuta nafasi mbili za juu”
alimaliza.
0 comments:
Post a Comment