Friday, November 18, 2016

Arsene Wenger amedai kwamba kwenye kikosi chake ana wachezaji watatu ambao wanaweza kucheza nafasi ya Hector Bellerin kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Manchester United utakaopigwa Old Trafford Jumamosi wikiendi hii.

Bellerin, 21, aliumia kifundo cha mguu kwenye mchezo dhidi ya Tottenham ulioisha kwa sare ya bao 1-1 kabla ya kupisha wiki ya michezo ya kimataifa na atakuwa nje kwa wiki nne.

Lakini kuelekea mchezo huo, Wenger amesisitiza kuwa Carl Jenkinson, Gabriel na Francis Coquelin wote wanaweza kucheza nafasi hiyo.

Wenger pia ameongeza kuwa uwepo wa Shkodran Mustafi ni option nyingine katika nafasi hiyo, lakini ameondoa uwezekano wa kumchezesha beki huyo ili kutovuruga nafasi ya beki wa kati ambayo wakati huu imeimarika kwa kiasi kikubwa.

"Tuna wachezaji ambao wameshawahi kucheza michezo mingi tu ya Ligi ya England kama Jenkinson.

"Vile vile tunaweza kumchezesha Gabriel... na Coquelin ameshawahi kucheza pale.

‘[Shkodran] Mustafi ameshawahi kucheza pale pia. lakini nisingependa kuvuruga eneo la beki ya kati ambayo kwa sasa inafanya vizuri.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video