Tuesday, November 15, 2016

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba Zacharia Han Poppe amewaondoa hofu mashabiki wa klabu hiyo juu ya mshambuliaji wao kipenzi Laudit Mavugo na kuwasisitiza kutulia na kusubiri matunda mema kutoka kwa mshambuliaji huyo.

Hans Poppe amedai kuwa wao kama kamati watasikiliza tathmini ya kocha wao juu ya mchezaji huyo halafu watajua nini hasa cha kufanya.

Mavugo ambaye ni raia wa Burudi hivi karibuni amekuwa akipata wakati mgumu baada ya kucheza michezo mfululizo bila ya kutikisa nyavu za wapinzani kinyume na matarajio ya mashabiki wengi wa klabu yake.

"Tutamsikiliza kocha tuone anasemaje, inaweza kuwa bado lakini ni mtu ambaye anaonekana ata-improve (ataimarika) kama unavyojua huyu (Mavugo) hajafanya pre-season, kwa hiyo inawezekana akawa tofauti na wenzake, hivyo kocha anaweza kuendelea kumpa nafasi lakini yote kwa yote tutamsikiliza kocha anatuambia nini," Hans Poppe amesema.

Hans Poppe ameenda mbali zaidi na kutolea mfano wa Okwi alipowasili kwa mara ya kwanza na kusema alicheza kwa takriban miaka mitatu bila kung'ara lakini baadaye akaja kuwa mchezaji tishio kwenye soka la hapa nchini.

"Ni kweli bado hajafurhisha lakini sio sababu ya kusema kwamba mtu akiwa anacheza hivyo basi aondoke kwasababu ukumbuke kwa mfano mchezaji kama Okwi (Emmanuel) amesikika sana siku hizi lakini alicheza Simba kama miaka mitatu kabla ya kuanza kusikika."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video