Friday, November 18, 2016

Antonio Conte amefichua kwamba Cesc Fabregas na Oscar wataendelea kubaki kunako klabu ya Chelsea.

Viungo hao wawili wamekuwa wakihusishwa na kuondoka klabuni hapo kuelekea usajili wa dirisha dogo mwezi Januari, wakielezwa kuwa mbioni kujiunga na vilabu vya Inter na AC Milan.

Hata hivyo, Conte hana nia ya kumwachia mchezaji yeyote kati ya wawili hao, dhumuni lake likiwa ni kubaki na kikosi kipana kitakachomsaidia kuwania ubingwa wa EPL msimu huu.

Alipoulizwa kuhusu Oscar, Conte aliwajibu waandishi: "Mustakabali wake bado uko Chelsea. Nimemaliza. Kwangu ni mchezaji muhimu sana kikosini. Ni mchezaji mzuri aliye kwenye kiwango bora."

Kuhusu hali ya Fabregas klabuni hapo, aliongeza: "Yupo katika hali nzuri na anaweza kucheza Jumapili kama ilivyo kwa Oscar."

Chelsea wanarejea kwenye kinyang'anyiro cha Premier League wikiendi hii wakiwa ugenini kukabiliana na Middlesbrough.

Chelsea walienda mapumziko kupisha michezo ya kimataifa wakiwa wameshinda mechi tano mfululizo na kufanikiwa kufunga mabao 16 bila kuruhusu hata bao moja.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video