Sunday, November 6, 2016

Hii mechi ukiitazama utahisi ya upande mmoja ila Azam FC ana kazi ya ziada kutafuta ushindi kwa mwenyeji wake leo katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 

Mechi nne za mwisho alizocheza Mbao FC, amefungwa mechi tatu na kutoka sare mechi 1 tu dhidi ya Tanzania Prisons ugenini (1-1). Amefungwa 3-0 na Yanga, 1-0 na Simba SC na kupigwa 2-0 na Kagera Sugar. Wapo nafasi ya 13 katika ligi wakiwa na pointi 13. Wana kiu kubwa ya kupanda juu . Watakubali kupoteza dhidi ya Azam FC ? Uwanja wa nyumbani?

Ukiwatizama Mbao FC kimbinu na kiufundi utaona ni kama timu ambayo ipo katika " pre season" na inajengeka vizuri taratibu kuanzia nyuma. 

Ujenzi wa timu huanzia kwenye backline kuja eneo la kiungo na mwisho katika ushambuliaji. 

Mbao mwanzo wa ligi walikuwa kapu la magoli na wakicheza kidhaifu sana idara zote lakini kadri muda unavyokwenda wanajengeka vizuri na wanatoa upinzani mzuri kwa wenzao ingawa wana makosa mengi kiufundi kuliko kimbinu na kimfumo. 

Mbao wanacheza vizuri ndani ya dakika 30 mpaka 40 wakiwa vizuri kwenye kujilinda na kujenga mashambulizi ya kushitukiza lakini mapungufu makubwa toka eneo la kiungo kwenda mbele linawafanya kushindwa kukaa na mpira mbele na kujikuta muda mwingi wanapoteza mipira na kuingia katika utumwa wa kukaba ambao unawachosha na mwisho wa siku kukosa umakini. 

Wanakosa wachezaji wazoefu wenye uwezo binafsi kuusoma mchezo na kuubadili ili kusaka magoli kwenye offensive patterns. 

Wanakutana na Azam FC waliopo kwenye " tactical and technical build up" na wapo katika hatua nzuri baada ya kusuasua mwanzoni. 

Michezo minne ya mwisho, Ameshinda michezo mitatu na kwenda sare mchezo mmoja dhidi ya Mtibwa Sugar. Ameshinda 1-0 dhidi ya Toto, 3-2 dhidi ya Kagera na 1-0 dhidi ya JKT Ruvu. Wapo nafasi ya 3 wakiwa na pointi 22. 

Walianza vibaya ligi na kujikuta wakipoteza zaidi ya pointi 17 baada ya kufungwa mechi 3 sawa na pointi 9 na kutoa sare 4 sawa na kupoteza pointi 8.

Majeruhi katika safu yao ya ulinzi , kuondoka kwa Kipre na kubadilishwa kwa benchi la ufundi ni sababu za kufanya vibaya .

Mbao wana kazi ya ziada leo kuwazuia Azam FC katika saikolojia hii ya kutaka kupanda juu kuusaka ubingwa wa ligi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video