Thursday, November 10, 2016

Leo ndio ilikuwa mechi ya mwisho kwa Kocha Mkuu wa Yanga SC Hans Van Pluijm kuliongoza benchi la ufundi la timu hiyo kama kocha mkuu. 

Kocha huyo atampisha mzambia George Lwandamina kuiongoza klabu hiyo katika mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara utakaoanza Disemba 17 baada ya dirisha dogo la usajili. 
   
Tuziangalie tofauti zao waalimu hawa wawili toka mwaka 2014 mpaka mwaka huu 2016 katika vilabu vyao. 

Tukianza na Hans Van Pluijm, ameiongoza Yanga SC katika mechi 117 katika mashindano yote . Ameshinda mechi 74 na kutoa sare 23. 

Hans Van Pluijm anaesifika kwa mfumo wa kidachi wa Total Football, katika mechi hizo 117 amepoteza mechi 23 tu na kuiweka vyema klabu hiyo ya mtaa wa jangwani katika ramani ya soka la Tanzania na Afrika kiujumla baada ya kuiwezesha timu hiyo kunyakua makombe mawili ya ligi kuu 2014-15 & 2015-16 , Kombe la FA 2016 na kuifikisha Yanga SC raundi ya pili klabu bingwa ilipotolewa na Al Ahly na kuangukia michuano ya Shirikisho Afrika na kuishia hatua ya nane bora. 

Hans pia anashikilia tuzo ya kocha bora wa ligi kuu Tanzania bara 2015-16. 

George Lwandamina ; kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka huu 2016 alipojiuzulu kuifundisha Zesco United , ameiongoza katika mechi 113 akishinda mechi 69! .

George Lwandamina mwalimu mwenye falsafa ya kupenda soka la vijana , katika mechi hizo 113 amepoteza mechi 27 na kwenda sare mara 17 . Ni moja ya matokeo mazuri ndani ya Zesco United inayoshiriki ligi kuu nchini Zambia . 

Ameipa Zesco United ubingwa wa ligi kuu mara mbili mfululizo mwaka 2014 na 2015 pia akaiwezesha timu hiyo kuibuka maningwa wa kombe la Barclays nchini humo mwaka 2014. 

Ubora wa George Lwandamina mwaka 2014 na 2015 ulimfanya kuchaguliwa kocha bora wa Zambia 2014-15 hali iliyompa tiketi ya kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo. 

Ukitazama waalimu wote hawa mafanikio yao yanashabihana . Lwandamina akibeba kombe la ligi kuu mara mbili sawa na Hans Van Pluijm, Barclays Cup kwa Lwandamina na FA Cup kwa Hans Van Pluijm. Wote wana vikombe vitatu kabatini.

Samuel Samuel

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video