Wednesday, November 2, 2016

Mbeya  City wameshinda kwa mara ya kwanza katika mechi saba walizokutana na Yanga tangu wapande Ligi kuu Soka Tanzania Bara msimu wa 2013/2014
 Imeandikwa na Mchambuzi wa soka, Samuel Samuel

MBEYA CITY
Hongera kwake Kina Phiri aliisoma vyema Yanga SC na kutumia makosa yao kuibuka na ushindi.
  Ukiona kikosi cha Yanga kimetoka na eneo la kiungo cha chini amesimama Mbuyu Twite basi " mpango kimbinu " ( tactical approach ) wa Yanga SC ni kuziba eneo la kati kwa mipango ya kujilinda hususani wanapokutana na timu zinazokamia au zenye viungo wazuri . Approach hii hufungua wings za Yanga SC kusimamia mipango yote ya mashambulizi.
   Kina Phiri alilijua hili vyema . Alichofanya ni kitu rahisi tu , kujaza viungo wengi kati kumlazimisha Mbuyu Twite kucheza mstari mmoja na walinzi wa kati kama " deep lying holding midfielder" . Dhumuni kimbinu kukata kombinesheni yake na Haruna Niyonzima hali iliyowafanya Yanga kuwaongezea eneo la kupanga mashambulizi yao mbele ya Yanga.
  Mpango wa pili aljipanga kupangua mipango ya mashambulizi ya Yanga SC kupitia " flanks" hususani kwa Saimoni Msuva kulia.
  Aliwatumia full backs wake kina Mwasapili kupanda juu kwa kasi kuzuia uwezekano wa full  backs na wings za Yanga kupanda. Hili walifanikiwa na ndio maana Yanga wakawa wanapiga squre passes nyingi na mipira mirefu kupitia Niyonzima nje ya mchezo wao wa pasi nyingi na kasi ya kwenda kwa sababu Mbeya City waliziba njia.
  Mpango wa tatu ambao ulifanikiwa mapema , ni kuwatoa Yanga mchezoni na kuwalazimisha kucheza faulo ndani ya 30 yao ( final third ) ili watumie mipira iliyokufa kufunga. Faulo ya Mwasapili dakika ya 6 kwa makosa ya Dida kujipanga langoni yanaipa Mbeya City goli.
  Nguvu na kasi muda wote ulikuwa mtaji mzuti kwa Kina Phiri dhidi ya Yanga ambao hakuwa na kasi kama ilivyo kawaida yao.

YANGA SC

Mipango ya kumtumia Mbuyu Twite kama kiungo wa chini kwenye mechi ya kukamia kama hii ya leo ilikuwa safi lakini kucheza chini ya kiwango kwa Vicent Bossou na kumfanya Andrew Vicent kuhaha kucheza juu ya mstari wa marking kulia na kushoto kulimlazimisha Twite kushuka chini na timu kukaribisha mashambulizi ya mara kwa mara.
  Mwinyi Haji alikuwa anapanda juu na kushindwa kumdhibiti vyema Ditram Nchimbi kitu ambacho kilimfanya Dante kuvutika kushoto na Twite kujaribu kumpa back kitu ambacho kiliwafanya Mbeya kuwa na " direct contact " na Dida ndio maana wamepiga mashuti mengi ya mbali langoni mwa Yanga. ( long ranges )
   Sub ya kwanza kuifanya kwa Hans Van Pluijm ilitakiwa kumtoa Bossou na kumwingiza Kelvin Yondani . Yondani licha kucheza kama mlinzi wa kati pia ana uwezo wa kusogea juu na kusaidia kukaba kati na kujenga mashambulizi tokea nyuma.
   Ni msifu kocha wa Yanga kipindi cha pili baada ya kugundua timu inakosa muunganiko mzuri kati na pembeni kwa kuwatoa Mbuyu Twite kumwingiza Kamusoko kucheza kama " defensive midfielder " kuitoa mipango ya kushambulia kutokea pembeni baada ya Mbeya City kuziba na kujenga muunganiko wao mzuri na Haruna Niyonzima kuifanya timu kushambulia kipitia kati kwa " give and go passes ". Ukitazama kipindi cha pili waliwatuliza vizuri Mbeya City sema walishindwa kurudi mchezoni kwa tension na pressure ya mchezo kutanguliwa goli mbili mbele na Mbeya City.
  Mabadiliko ya Mwashuiya kwa Kaseke hayakuwa na faida upande wa kuongeza mashambulizi ya upande au kutengeneza krosi nzuri kwa Chirwa na Ngoma. Mwashuiya hakuwa aggresive kushambulia wala kutengeneza pasi nzuri za mwisho na hii ni mechi ya tatu akiingia kama plan B anashindwa kufikia malengo .
  Kwa ujumla Yanga kwa zaidi ya asilimia 40 hawakuwa na mipango mizuri katika safu ya ushambuliaji.

MWAMUZI

Dakika 15 za mwanzo aliumudu vyema mchezo lakini taratibu alianza kutoka mchezoni kwa maamuzi ya utata.
Goli la pili la Mbeya City , anawaita wachezaji wa Yanga wajipange baada ya kuhesabu hatua za ukuta ghafla wachezaji wa Mbeya City wanaanzisha mpira na kupata goli. 

Chanzo cha utata;

Alisimama kuwapanga Yanga lakini makosa ya Mbeya  City kuanzisha mpira haraka anayakubali . Baada ya kuzongwa na wachezaji wa Yanga anakubali amekosea na kulikataa gol lakini baada ya kuzongwa tena anakubali lilikuwa goli. Hiki ni kituko cha mwaka kwenye soka letu.
Ni bora angesimamia maamuzi yake ya kwanza kuliko kukubali na kukataa tena . Niliwahi kuandika makala gazeti la " Mtanzania " TFF waangalie upya kiwango cha taaluma kinachotolewa kwa waamuzi wetu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video