Thursday, November 10, 2016

Tofauti na mechi zote walizowahi kukutana Ruvu Shooting na Yanga SC , leo vijana wa Ruvu Shooting walionesha ushindani na kutulia vyema. 

Goli la mapema dakika ya 6 liliwajenga vyema kisaikolojia na kuonesha nidhamu nzuri ya mchezo hususani ukabaji na kufanya mashambulizi machache yenye akili. 

Uzoefu na ubora wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC umewafanya kupoteza mechi hii. Yanga SC toka itoke Mbeya kucheza na Prisons imekuwa na muda mzuri kupumzika na kufanya mazoezi tofauti na Ruvu Shooting ambao walikuwa safarini juzi na kuomba mechi yao isogezwe mpaka leo lakini wameonesha stamina nzuri dakika zote 90 .

Yanga SC dakika 20 za mwisho wa mchezo walipoa na kuonekana kuchoka hali iliyowafanya Ruvu Shooting kufika sana langoni mwao. Umakini mdogo kwenye kushambulia na kudra za mpira kugonga mwamba zimeokoa jahazi la jangwani. 

Mchezo ulikuwa mzuri sio wa upande mmoja kama ulivyotarajiwa ingawa Haruna Niyonzima anabeba asilimia 70 za kuutawala mchezo huu. Alikuwa bora na kuichachafya vyema ngome ya Ruvu Shooting.

Dakika ya 36 juhudi binafsi zinamfanya amtengenezee pasi nzuri Saimoni Msuva na kuisawazishia Yanga SC baada ya Abdulahman Musa kuwatanguliza mbele Ruvu Shooting dakika ya 6 ya mchezo kwa goli zuri wing ya kulia baada ya kuachia mkwaju mfupi uliomshinda kipa Beno Kakolanya na kutinga wavuni. 

Dakika ya 56 Haruna  akipokea pasi toka kwa Donald Ngoma aliyeangushwa chini ndani ya 18 lakini akaweza kumsogezea Haruna Niyonzima aliyeachia kombora zuri na mpira kutinga nyavuni, hii inathibisha ubora wa kiungo huyo katika mchezo huu. 
  
Samuel Samuel

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video