Hassan Kessy |
Msuluhishi wa kisheria wa sakata la madai ya Simba dhidi ya Young
Africans hali kadhalika Mchezaji Hassan Hamisi Ramadhani maarufu kama
Hassan Kessy, Wakili Msomi, Mzee Said El-Maamry anatarajiwa kukutana na
pande zinazopingana Alhamisi Novemba 3, mwaka huu ili kufikia mwafaka wa
mwadai hayo.
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iliagiza pande za
Simba na Young Africans kumaliza suala hilo mapema mwezi uliopita,
lakini kwa sababu zilizo nje ya TFF na Kamati yake walishindwa kufanya
hivyo kupewa barua ya wito kuitwa kikaoni Oktoba 29, mwaka huu.
Hata hivyo, msuluhishi huyo alishindwa kuendelea na kikao hicho baada
ya taarifa kutoka Young Africans kusema kwamba mmoja wa Wawakilishi
wake, Wakili Msomi Alex Mgongolwa kuwa safarini Iringa alikokwenda kwa
sababu ya matatizo ya kifamilia. Ilielezwa kuwa Mgongolwa ambaye ni
Mwanasheria wa Young Africans, alifiwa hivyo kuomba kupangiwa siku
nyingine.
Kutokana na hali hiyo, E-Maamry amepanga sasa kukutana nna viongozi
na/ au Wawakilishi wa pande zote mbili Alhamisi saa 11.00 jioni kwenye
ofisi za TFF ili kuketi chini ya kuangalia namna ya kumaliza madai ya
Simba iliyowasilisha mashauri mawili ambako moja ni dhidi ya Young
Africans ilihali jingine ni dhidi ya mchezaji Hassan Kessy.
Mzee El-Maamry amesema: “Ili kutenda haki, lazima tutoe nafasi kwa
pande zote kusikiliszwa. Ni vema Mwanasheria wa Young Africans
akasubiriwa.”
Kamati ya TFF inasuburi makubaliano hayo, na ikitokea imeshindikana,
suala hilo litarudi kwenye Kamati hiyo kwa ajili ya uamuzi wa mwisho kwa
mujibu wa taratibu, kanuni na sheria zinazoongoza mpira wa miguu.
0 comments:
Post a Comment