Goli la dakika za majeruhi la Marten de Roon liliipa pointi moja muhimu Middlesbrough walipokuwa ugenini katika Uwanja wa Etihad dhidi ya Manchester City.
Sergio Aguero aliwapa City goli la uongozi, baada ya kuunganisha mpira mzuri wa Kevin de Bruyne na kufunga goli lake la 150 tangu ajiunge klabuni hapo.
Dondoo muhimu za kufahamu
- City wametoka sare michezo mitatu ya nyumbani mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2009 wakati Mark Hughes alipokuwa kocha wa klabu hiyo.
- Aguero amezifunga timu 28 kati ya 30 tofauti tofauti alizokutana nazo kwenye Ligi Kuu ya England.
- Tangu acheze mchezo wake wa kwanza Premier League Septemba 2015, De Bruyne ametoa pasi za magoli 19 kwenye michuano yote kwa Man City, sita zaidi ya mchezaji yeyote.
- Middlesbrough wameshinda mchezo mmoja tu wa ugenini wa Premier League kati ya 19 waliyocheza (sare mara 5, wamefungwa mara 19).
0 comments:
Post a Comment