Thursday, November 10, 2016

Kiungo mshambualiji wa Yanga Haruna Niyonzima ametoa shukrani zake za dhati kwa mashabiki kwa sapoti kubwa waliyowapa hali iliyopelekea kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Niyonzima aliyekuwa nahodha kwenye mchezo wa leo ambaye pia ndiye aliyefunga bao la ushindi ameongeza kuwa wanaamini watafanya makubwa zaidi mzunguko wa pili hasa baada ya kufanikiwa kupunguza pengo na kubakisha alama 2 dhidi ya vinara Simba SC.

"Tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa matokeo ya leo, limebaki pengo la pointi 2 tu kama nilivosema awali huu ni mzunguko wa kwanza tu. Mashabiki na wapenzi wa Yanga wategemee mazuri mzunguko wa pili maana sasa tutapata muda wa kupumzika na kujipanga zaidi," alisema.

Akizungumzia taarifa za kuondoka kwa kocha wao kipenzi Niyonzima amesema:"Tulimzoea mwalimu Hans (van der Pluijm), lakini huu ndiyo mpira na hizi ndizo moja ya changamoto zake, kitu kikubwa ni kuwa tupo tayari kufanya kazi na mwalimu mpya."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video