Thursday, November 10, 2016

Yanga wamefanikiwa kumaliza vyema mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwa kuwandika Maafande wa Ruvu Shooting kwa mabao 2-1, mchezo uliofanyika katia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali kwa dakika zote tisini, Ruvu Shooting waliannza kupata bao mapema tu dakika ya 7 kupitia kwa mchezaji wao Abdulrahman Musa baada ya kugongeana kwa umaridadi na kuwahadaa mabeki wa Yanga kabla ya kuutumbukiza mpira huo wavuni.

Goli hilo la lilikuwa ni kama limewatibua, Yanga baada ya kuanza kusakata soka la kasi lililoambatana na pasi nyingi na za haraka wakiwa na lengo moja tu la kusawazisha na pengine kuongeza bao.

Harakati hizo za Yanga hatimaye zilizaa bao dakika ya 31 kupitia kwa Simon Happygod Msuva baada ya kuunganisha krosi maridadi kutoka kwa Haruna Niyonzima aliyemhadaa kwa umahiri mkubwa beki wa Ruvu Shooting.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoshana nguvu na kwenda kupokea mawaidha kutoka kwa makocha wao.

Mapema hata kabla ya kipindi cha pili kuanza kocha wa Yanga Hans van der Pluijm alipewa adhabu ya kuondoka kwenye benchi na kwenda kukaa jukwaani kwa mashabiki kwa kile kinachodaiwa kutoa lugha isiyo na stara kwa mwamuzi wa mchezo huo.

Tukio hilo halikuwazuia Yanga kuendelea kucheza soka la kushambulia zaidi na kufanikiwa kuandika bao la pili dakika ya 57 kwa shuti kali kutoka kwa Haruna Niyonzima, ambaye alipata pasi iliyopigwa kwa ugumu na Donald Ngoma ambaye wakati huo alikuwa ameanguka chini.

Ushindi wa leo unaendelea kuibakisha Yanga kwenye nafasi yake ua pili lakini wakifikisha alama 33, tofauti ya pointi mbili nyuma ya vinara Simba ambao jana walipoteza mchezo wao dhidi ya Maafande wa Tanzania Prisons ya jijini Mbeya.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video