Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), limemteua Jonesia
Rukyaaa - Mwamuzi wa soka kutoka Tanzania kuwa miongoni mwa waamuzi wa
kati 10 watakaochezesha mechi za Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika
kwa wanawake zitakazofanyika kwa wiki mbili kuanzia Novemba 19, mwaka
huu.
Kwa uteuzi huo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
amempigia simu Jonesia kumpongeza kwa hatua hiyo ambayo ni sehemu kubwa
ya mafanikio ya soka la Tanzania kufanya vema katika medani za
kimataifa.
Rais Malinzi amesema kwamba Mwamuzi Jonesia ameliletea heshima taifa
la Tanzania kwa kujijengea heshima ya kuaminika mbele ya Kamati ya
Ufundi ya CAF – Waratibu na Waandaaji wa fainali hizo zitakazofanyika
Cemaroon ambako mechi za mechi ya mwisho ya fainali itafanyika Desemba
3, mwaka huu.
“Namtakia kila la kheri, naamini kwamba Jonesia atafanya vema. Nina
uhakika kwamba hii ndiyo njia yake pekee ya kufanikiwa zaidi kwani ipo
siku atateuliwa kuchezesha hata fainali za Kombe la Dunia,” yalikuwa ni
maneno ya Malinzi akimwelezea Jonesia kwenye simu leo mchana.
Jonesia anafanya idadi ya waamuzi watakaochezesha mchezo huo kutoka
nchi za Afrika Mashariki kuwa watano kwani wengine kwa mujibu wa orodha
ya CAF ni Salma Mukansanga (Rwanda), Lydia Tafesse (Ethiopia), Carolyne
Wanjala (Kenya) na Suan Ratunga (Burundi).
Waamuzi wengine ni Maria Packuita wa Mauritius, Gladys Lengwe
(Zambia), Akhona Zennith Makalima (Afrika Kusini), Jeanne Ekoumou
(Cameroon) na Aissata Amegee (Togo). Katika orodha hiyo pia yumo Mary
Njoroge wa Kenya ambaye mwamuzi wa pembeni pekee.
Katika fainali hizo, timu shiriki ni Cameroon, Afrika Kusini, Misri
na Zimbabwe zipo kundi A wakati Nigeria, Ghana, Kenya na Mali zimo kundi
B.
Jonesia ambaye jana Jumanne
alirejea kutoka Cameroon kwenye kozi ya uamuzi ngazi ya juu, kesho
Alhamisi anatarajiwa kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara pale Mtibwa Sugar ya Morogoro itakapokaribishwa na
Mwadui kwenye Uwanja wa Mwadui. Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbao
Fc na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment