Monday, November 7, 2016

Team Manager wa Zesco United amethibitisha kuwa, kocha mkuu wa klabu yao George Lwandamina amejiuzulu nafasi yake lakini hajataoa sababu yeyote ya kufanya hivyo

“Ni kweli Lwandamina amejiuzulu. Tumepokea email yake leo asubuhi lakini hajataja sababu yeyote ya msingi ya kufikia uamuzi huo,” amesema Banda ambaye ni manager wa Zesco United.

klabu ya Zesco imetoa taarifa rasmi kupitia ukurasa wao wa facebook wakithibitisha kuachana na kocha huyo ambaye wiki chache zilizopita alikuwa Dar es Salaam na kuhusishwa kutaka kujiunga na klabu ya Yanga hadi kupelekea kocha mkuu wa Yanga kutangaza kujiuzulu.

“Kocha mkuu wa Zesco United George Lwandamina amejiuzulu nafasi yake asubuhi ya leo, klabu imepokea na kuikubali barua yake ya kujiuzulu na kumshukuru kwa mchango wake pamoja na kazi yake aliyoifanya akiwa kocha wa Zesco United,” inasomeka taarifa ya Zesco United iliyotolewa kupitia ukurasa wao wa facebook.

Lwandamina alijiunga na Zesco mwaka 2004 na kufanikiwa kushinda mataji mawili ya ligi, kombe moja la Barclays, Ngao ya Jamii na kuiongoza timu hadi hatua ya nusu fainali ya CAF Champions League mwaka 2016.

Klabu imemteua aliyekuwa  kocha msaidizi Tenant Chembo kuchukua nafasi ya Lwandamina hadi mwisho wa msimu huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video